Asasi hii ilianzishwa hapa Musoma kuanzia mwezi Februari mwaka 2011 ikiwa
na wanachama waasisi kumi (10). Wazo la kuanzisha Asasi hii lilitokana na
ukweli kwamba moja ya vikwazo vinavyosababisha kudorora kwa maendeleo katika
jamii za nchi zinazoendelea ni kukosekana kwa taarifa sahihi na za wakati.
Asilimia kubwa ya jamii ya Watanzania wanaishi nje ya miji ambako kuna uhaba wa
vyombo vya kupashana habari kama vile magazeti, radio, luninga, internet n.k.
Kukosekana kwa taarifa za mambo yanayofanyika ndani ya jamii na nje ya jamii
waliyomo kunawanyima fursa ya kushiriki katika kukabiliana na changamoto
mbalimbali za kijamii, kiuchumi na kiutamaduni ili kwenda na mabadiliko katika
dunia ya leo ya sayansi, tekinolojia na utandawazi.
DIRA
Kuwa na jamii yenye uelewa mpana wa habari sahihi za masuala ya
kijamii, kiuchumi na kiutamaduni na kutambua mabadiliko yanayotokea kati yake
na jamii zingine ili kukabiliana na changamoto za kimaendeleo.
DHAMIRA
Asasi inadhamiria kushiriki na kushirikisha ngazi zote za kijamii hasa
makundi yaliyoko pembezoni katika ukusanyaji, uandikaji, usambazaji na
upashanaji habari.
MADHUMUNI
Kuhabarisha jamii jinsi ya
kukabiliana na changamoto za athari na madhara umasikini,
Rushwa na VVU/UKIMWI.
Kushirikisha jamii katika
ukusanyaji wa taarifa muhimu, kuziandika na kuzisambaza ili
Kuimarisha mawasiliano ya
habari.
Kuimarisha mitandao ya mawasiliano ndani ya jamii ili jamii iweze
kupata taarifa sahihi
Zinazoendana na wakati.
Kushirikisha jamii katika kuibua
changamoto na kukuza ushawishi na utetezi wa sera
Mbalimbali kwa njia ya midaharo ili
ziwe na tija kwa jamii.
Kufanya tafiti mbalimbali za masuala ya
kijamii, kiuchumi na kiutamaduni ili kuzipatia
Ufumbuzi.
Kuyajengea uwezo makundi mbalimbali ya kijamii Kwa njia ya vipeperushi,
magazeti,
Radio, TV na mafunzo ili kupata
ufahamu wa kujiletea mabadiliko.
Kukuza uelewa wa jamii juu ya kutambua na kutetea haki zao za msingi
zinazokiuka Misingi ya demokrasia,
usawa, utawala bora, uwazi na uwajibikaji.