Karibu Musoma Information Center kwa huduma zifuatazo:- 1) Kwa kutengenezewa design mbalimbali kama za Business card, Vipeperushi, mabango mbalimbali, kadi za Harusi za kisasa zaidi, kadi za mialiko mbalimbali, Vitambulisho vya wanafunzi wa sekondari na katika kampuni mbalimbali ( ID cards) na kadi nyinginezo zenye design ya kuvutia. 2) Kutengenezewa mabango ( Posters) mbalimbali zinazohusu biashara ya mhusika au bidhaa mbalimbali. 3) Kutengenezewa nembo ( LOGO) za kuhusiana kampuni au biashara yako. 4) Tunatengeneza tovuti ( Websites ) zenye kiwango ambacho huwezi amini kama zinatengenezwa musoma, kwa bei nafuu ambayo huwezi ipata kwingine isipo kuwa kwetu. 5) Mwisho tunatoa ushauri na elimu kuhusiana na maswala ya computer.5) Sisi ni watengenezaji wa blog zinazokaa mfumo wa website. kama hii unayoiona.

News

WAZAZI NA WALEZI WATAKIWA KUWAPELEKA WATOTO WAO WALIO NA UMRI CHINI YA MIAKA 5 KWENDA KUPATA CHANJO KATIKA VITUO VYA AFYA

   
MKUU WA MKOA WA MARA JOHN TUPPA



Na Shomari Binda
         Butiama,

WAZAZI na Walezi walio na Watoto wenye umri chini ya Miaka 5 wamehimizwa kuwapeleka katika vituo vya zahanati watoto wao kupata chanjo ili kuepukana na maradhi yanasosababisha vifo vingi vya watoto ili kufikia malengo ya melinia namba 4 ifikapo Mwaka 2015.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mara John Tupp katika hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya ya Butiama Angelina Mabula kwa niaba yake katika uzinduzi wa chanjo ya kuzuia ugonjwa wa kuhara na nimonia uliofanyika katika kata ya Kukirango  Wilayani Butiama na kuhudhuliwa na wataalamu wa afya na viongozi wa Serikali Mkoani Mara.

Alisema malengo ya melenia namba 4 na 5 ya Kimataifa ambayo Tanzania imeridhia yanahusu kupunguza vifo vya akina mama na watoto wakati wa uzazi na watoto walio na umri chini ya miaka 5 ambavyo vimekuwa vikitokea kwa wingi na kupelekea kupunguza nguvu kazi ya Taifa.

Tuppa alisema malengo ya melenia na Mkukuta yaliyotafsiriwa katika Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) yamelenga kupunguza vifo vya watoto walio na umri chini ya miaka 5 toka 81 vya sasa hadi 54 katika kila watoto 1,000 wanaozaliwa na vifo vya watoto chini ya mwaka mmoja toka 32 vya sasa hadi 19 kila watoto 1,000 waliozaliwa hai ifikapo Mwaka 2015.

Alisema idadi ya magonjwa yanayokingwa kwa chanjo imeendelea kuongezeka toka chanjo chanjo dhidi ya maradhi manne hadi tisa kufikia mwaka 2009 na kusema chanjo ya magonjwa ya kuhara na nimonia iliyozinduliwa inafanya maradhi yanayokingwa kwa chanjo kufikia 11.

"Magonjwa mengine yanayokingwa kupitia mpango wa Taifa wa chanjo ni kifua kikuu,ugonjwa wa Polio,Surua,kifaduro,Pepopunda,Dondakoo,Homa ya ini pamoja na Homa ya uti wa mgongo.

"Nachukua fursa hii kutoa wito kwa Wananchi wa Mkoa wa Mara na Watanzania kwa ujumla wawwapeleke Watoto kwenye vituo vya kutolea Huduma ya chanjo ili kwakinga na maradhi haya na kubolesha maisha ya watu na uchumi wetu,"ilisema sehemu ya hotuba hiyo.

Alisema pamoja na Serikali ya Tanzania kuhakikisha watoto wote walio na umri chini ya mwaka mmoja wanapata chanjo lazima ifahamike gharama ya chanjo hizo ni kubwa ambapo kila mtoa huduma,mzazi,mlezi viongozi pamoja na Wananchi wote kutambua gharama hizo.

"Gharama ya mtotot mmoja ni shilingi 51,218.85 kwa chanjo zote ambazo mtoto anazipata gharama ambazo hazijajumuisha kutoka kiwandani hadi kituo cha kutolea huduma ,gharama ya mabombaya sindano na mitungi ya gasi hivyo basi utaona Serikali ya Tanzania inavyotumia gharama kubwa kuokoa maisha ya watoto wanaozaliwa,"alisema.

Aidha Wazazi,Walezi pamoja na wanajamii wametakiwa kutambua kuwa jukumu la kuhakikisha kila mtoto anayezaliwa anapata chanjo kama haki stahiki ikiwa ni pamoja na kupelekwa katika vituo vya kutolea huduma ya chanjo mbalimbali na huduma zingine ambazo zimekuwa zikitolewa kwa watoto.

Katika taarifa ya Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mara Dokta Samsoni Wenani ilisema idadi ya watoto waliopata chanjo imeongezeka kutoka asilimia 81 mwaka 2009 hadi asilimia 90 mwaka 2012.

Alisema chanjo pamoja na vifaa viligawiwa na kusambazwakatika Wilaya zote za Mkoa wa Mara Mwaka 2012 huku Mkoa ukiwa na lengo la kuchanja watoto chini ya Mwaka mmoja wapatao 91,062 katika kipindi cha Januari hadi Novemba 2012 ambapo watoto walipatiwa chanjo mbalimbali.


DEREVA BODABODA ACHINJWA KISHA KUNYANG'NYWA PIKIPIKI NA KUTUPWA VICHAKANI

MADEREVA WA PIKIPIKI WAKIPITA KATIKA BARABARA YA MKENDO KWENDA KUMSHUHUDIA MWENZAO HOSPITALI YA MKOA WA MARA

MWENZAO ACHINJWA

BODABODA WAKIWA NJE YA HOSPITALI YA MKOA WA MARA

WANANCHI WAKISHUHUDIA MWILI WA BODABODA ANYEDAIWA NI MKAZI WA KIGERA KIARA ALIYECHINJWA NA KUNYANG'ANYWA PIKIPIKI


SEHEMU YA MGUU AMBAO PIA ULIKATWA NA MAPANGA


ASKARI POLISI WAKIWAPA NAFASI WANANCHI KUUTAMBUA MWILI HUO UKIWA NDANI YA GARI


DAKTARI AKIWA KAZINI KABLA YA KUPELEKWA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI

MWILI WA DEREVA WA PIKIPIKI MAARUFU KAMA BODABODA ALIYECHINJWA NA KUNYANG"ANYWA PIKIPIKI ULIOKOTWA KATIKA MAENEO YA NYANKANGA NJE KUDOGO YA MJINI WA MUSOMA UKIPELEKWA KATIKA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI HOSPITALI YA MKOA WA MARA.
         Nb;tunaomba radhi kwa baadhi ya picha ya tukio hili

Askari polisi wanaohudumia kitengo cha dawati la Jinsia Wanawake na Watoto wametakiwa kuwa na kauli nzuri wanapokuwa wanawahudumia wahanga wanaofanyiwa vitendo vya ukatili wanapowafikia.

SHUKA CHINI KWA PICHA NA MAELEZO ZAIDI


WANAFUNZI WA TARIME HIGH SCHOOL

WAUMINI WA KANISA LA ANGLICAN NAO HAWAKUWA NYUMA

POLISI WAKIWA KATIKA MAANDAMANO YA MAAZIMISHO YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA WILAYANI TARIME

WATOTO WANAFUNZI WA SHULE NAO WALISHIRIKI

KAIMU KAMANDA ZACHARIA AKIFAFANUA JAMBO


ASKOFU WA KANISA LA ANGLICAN DAYOSISI YA TARIME DK.MWITA AKILI AKISOMA HOTUBA KATIKA UFUNGUZI WA OFISI YA DAWATI LA JINSIA NA MAAZIMISHO YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

KAIMU KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM YA TARIME RORYA SEBASTIAN ZACHARIA KUSHOTO KATIKA MAAZIMISHO YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA NA UZINDUZI WA OFISI YA DAWATI KITUO CHA POLISI WILAYANI TARIME
Na Shomari Binda,Tarime
Askari polisi wanaohudumia kitengo cha dawati la Jinsia Wanawake na Watoto wametakiwa kuwa na kauli nzuri wanapokuwa wanawahudumia wahanga wanaofanyiwa vitendo vya ukatili wanapowafikia.
Kauli hiyo ilitolewa na Askofu wa Kanisa la Anglicana Dayosisi ya 
 Tarime Dk.Mwita Akili alipokuwa akifunga siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijnsia sambamba na ufunguzi wa Ofisi ya dawati la Jinsia katika kituo kikuu cha Polisi Wilayani Tarime
Alisema wahanga wa Ukatili hawana budi kuzungumza nao kwa unyenyekevu ili waweze kuelezea kwa umakini yale yaliyowasibu na si vyema kuzungumza nao kwa kuwafokea na kuendelea kuonekana wanyonge.
Askofu Mwita alisema kuanzishwa kwa dawati la Jinsia na ufunguzi  wa Ofisi hiyo kuwe ni chachu ya kuwasaidia Wanawake hasa wale wanaokutana na vitendo vya ukatili pale wanapowafikia kutaka msaada kutoka kwao.
“Watakaowafikia katika ofisi hii ni sawa na mama zenu,dada ama ndugu kwenu hivyo wasaidieni kwa kuzingatia maadili ya kazi na kuwa na moyo wa huruma ili wapate faraja na msifanye kinyume na hivyo.
“Mtu anaye kutana na suala la ukatili anahitaji msaada na kuwa naye kwa ukaribu naamini askari Polisi watakao kuwa katika dawati hili tayari wanayo mafunzo namna ya kuwahudumia wahanga wa Ukatili nawaombea kwa Mungu awape wepesi katikakutekeleza majukumu yenu ya kazi”,alesema askofu Mwita.    
Askofu Mwita alitumia nafasi hiyo kuihasa jamii kuachana na masula ya Ukatili hasa kwa Wanawake kwani wanapofanyiwa vitendo vya ukatili shughuli mbalimbali za kiuchumi zinakuwa hazifanyiki na hivyo jamii kuendelea kuwa masikini.
Alisema upo ukatili ambao hauzungumziwi sana katika jamii katika suala zima la kumnyima elimu Mwanamke na kudai kuwa hakuna ukatili mbaya kama huo kwani unakwamisha maendeleo.
“Mwanamke lazima apewe elimu pamoja na kumpa nafasi ya kumiliki mali ili aweze kufanya mambo ya faida katika jamii n asiwe Mwanamke wa kuomba kila kitu kwa Mwanaume ikiwa hata kama anataka kununua mafuta ya kupikia ama mboga,”alisema
Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Tarime Rorya Sebastian Zacharia alisema kutokana na askari wanaoshughulika na dawati kupata mafunzo ya namna ya kufanya majukumu yao anaamini watafanya kwa uadilifu mkubwa.
Alisema Jeshi la Polisi limeingia moja kwa moja katika mapambano ya ukatili wa Kijinsia na kudai kuwa jamii inapaswa kushirikiana na Jeshi hilo ili kuweza kutokomeza matukio ya ukatili katika jamii.
Like us on Facebook
Follow us on Twitter
Recommend us on Google Plus
Subscribe me on RSS