Karibu Musoma Information Center kwa huduma zifuatazo:- 1) Kwa kutengenezewa design mbalimbali kama za Business card, Vipeperushi, mabango mbalimbali, kadi za Harusi za kisasa zaidi, kadi za mialiko mbalimbali, Vitambulisho vya wanafunzi wa sekondari na katika kampuni mbalimbali ( ID cards) na kadi nyinginezo zenye design ya kuvutia. 2) Kutengenezewa mabango ( Posters) mbalimbali zinazohusu biashara ya mhusika au bidhaa mbalimbali. 3) Kutengenezewa nembo ( LOGO) za kuhusiana kampuni au biashara yako. 4) Tunatengeneza tovuti ( Websites ) zenye kiwango ambacho huwezi amini kama zinatengenezwa musoma, kwa bei nafuu ambayo huwezi ipata kwingine isipo kuwa kwetu. 5) Mwisho tunatoa ushauri na elimu kuhusiana na maswala ya computer.5) Sisi ni watengenezaji wa blog zinazokaa mfumo wa website. kama hii unayoiona.

HABARI KATIKA PICHA



 Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Matongo wakiangalia bwawa la Maji
 Baadhi ya wataalamu kutoka Mgodi wa North Mara wakifafanua Jambo kwa Waandishi wa Habari


KUHUSU JAMII INFORMATION NETWORK (JIN)

Asasi hii ilianzishwa hapa Musoma kuanzia mwezi Februari mwaka 2011 ikiwa na wanachama waasisi kumi (10). Wazo la kuanzisha Asasi hii lilitokana na ukweli kwamba moja ya vikwazo vinavyosababisha kudorora kwa maendeleo katika jamii za nchi zinazoendelea ni kukosekana kwa taarifa sahihi na za wakati. Asilimia kubwa ya jamii ya Watanzania wanaishi nje ya miji ambako kuna uhaba wa vyombo vya kupashana habari kama vile magazeti, radio, luninga, internet n.k. Kukosekana kwa taarifa za mambo yanayofanyika ndani ya jamii na nje ya jamii waliyomo kunawanyima fursa ya kushiriki katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za kijamii, kiuchumi na kiutamaduni ili kwenda na mabadiliko katika dunia ya leo ya sayansi, tekinolojia na utandawazi.
 
 DIRA
Kuwa na jamii yenye uelewa mpana wa habari sahihi za masuala ya kijamii, kiuchumi na kiutamaduni na kutambua mabadiliko yanayotokea kati yake na jamii zingine ili kukabiliana na changamoto za kimaendeleo.
 
DHAMIRA
Asasi inadhamiria kushiriki na kushirikisha ngazi zote za kijamii hasa makundi yaliyoko pembezoni katika ukusanyaji, uandikaji, usambazaji na upashanaji habari.   
 
MADHUMUNI
 Kuhabarisha jamii jinsi ya kukabiliana na changamoto za athari na madhara umasikini,  
 Rushwa na VVU/UKIMWI.
 
 Kushirikisha jamii katika ukusanyaji wa taarifa muhimu, kuziandika na kuzisambaza ili
 Kuimarisha mawasiliano ya habari.  
 
  Kuimarisha mitandao ya mawasiliano ndani ya jamii ili jamii iweze kupata taarifa sahihi
  Zinazoendana na wakati. 
 
 Kushirikisha jamii katika kuibua changamoto na kukuza ushawishi na utetezi wa sera 
 Mbalimbali kwa njia ya midaharo ili ziwe na tija kwa jamii.
 
  Kufanya tafiti mbalimbali za masuala ya kijamii, kiuchumi na kiutamaduni ili kuzipatia 
  Ufumbuzi.
 
Kuyajengea uwezo makundi mbalimbali ya kijamii Kwa njia ya vipeperushi, magazeti,
Radio, TV na mafunzo ili kupata ufahamu wa kujiletea mabadiliko. 
 
Kukuza uelewa wa jamii juu ya kutambua na kutetea haki zao za msingi zinazokiuka  Misingi ya demokrasia, usawa, utawala bora, uwazi na uwajibikaji.

JAMII YENYE UPENDO UFANIKIWA KWA KILA JAMBO

MKurugenzi wa Jamii Information Network akiongea na Marehemu Mwalimu James Irenge aliyewahi kumfundisha Hayati Mwl J.K Nyerere

VIJANA 200 KUJITAMBUA MKOANI MARA

ZAIDI YA VIJANA 200 KUJITAMBUA MKOANI MARA
Taasisi isiyo ya Kiserikali inayojishughulisha ya utoaji elimu  katka Masuala mbalimbali katika Jamii,kuibua changamoto na kusaidia Makundi yasiyojiweza ya Jamii Information Network (JIN)  inatarajia kuendesha  kongamano la vijana mjini hapa  mwaka  huu wa 2013.
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Mjini Musoma,Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Augustine Mgendi amesema Kongamano hilo linatarajia kufanyika huku likiwakutanisha Vijana zaidi ya 200 kutoka Shule 10 za Mjini hapa ambapo linalenga kuwajengea stadi za kujitambua,kujiamini na kujithamini.
Alisema katika Kongamano  hilo vijana hao watafundishwa kukabiliana na changamoto  zinazowakabili katika makuzi yao lakini pia  kuhamasisha Vijana kupambana na Ugonjwa wa  Ukimwi,kujifunza mbinu za  Ujasirimali,dhana ya kujiajiri na Changamoto zake  vijana kujenga Uzalendo,kupambana  na Umaskini,Rushwa ,Kuepuka Mimba za Utotoni katika Jamii.

   ‘Nadhani Vijana bado wanachangamoto kubwa sana katika kufanikisha ndoto zao na hii ni fursa pekee kwa Vijana kujifunza Mbinu mbalimbali maana tutakuwa na wataalam ambao wamebobea katika mambo hayo ili kutoa Mwanga kwa Vijana wetu ” alisema Mkurugenzi huyo
Mkurugenzi huyo alisema kuwa Shule zitakazoshiriki Kongamano hilo zitatajwa baadaye baada ya Mambo kadha wa kadha kukamilika
  “Ni Shule kumi zitakazoshiriki na mambo yakiwa tayari tutawafahamisaha ni shule gani ambazo tutakuwa nazo” alisema Mkurugenzi huyo
            
 Mkurugenzi huyo alisema kuwa watakuwepo wataalamu mbalimbali watakaohusika kutoa mafunzo katika Kongamano hilo huku akisema  kuwa Vijana ndiyo nguvu kubwa ya Taifa kwasasa hivyo wanahitaj miongozo ya Kimaisha katika kujitambua.
Kongamano hilo ambalo litakuwa linafanyika kila Mwaka litakuwa na kauli mbiu mbalimbali ambapo  alisema kwa Mwaka huu litakuwa na Kauli mbiu ya “Jitambue Kijana”  ambapo alisema kuwa Kongamano hilo litawasaidia  Vijana wengi  Kujitambua kutokana na Changamoto zinazowakabili kwasasa.
   “Tunatarajia Kongamano hili liwe linafanyika kila Mwaka ili kutoa elimu na mwongozo  wa kimaisha kwa vijana na kwa kuanza mwaka huu kauli mbiu yetu itafahamika kama  Jitambue Kijana  hii ni kutokana na vijana wengi  kutofikia Malengo yako kutona na Changamoto zilizopo”alisema  Bw Mgendi
Mbali na Kongamano hilo taasisi ya Jamii Information Network  ambayo hufanya shughuli zake mkoa wa Mara inatarajia kutoa elimu mbalimba mkoani Mara ili jamii huska kwenda na wakati kutokana asilimia kubwa ya Watanzania kuishi vijijini ambapo vyombo vya habari kufika inakuwa tabu.
Aidha Mkurugenzi huyo alisema kuwa  Taasisi hiyo inatarajia kutumia wanahabari mkoani Mara kuibua changamoto mbalimbali zilizopo vijijini ili kuziweka bayana na kufanya vipindi mbalimbali kutoka Vijijini ambavyo alisema vitaibua Changamoto zilizopo huko.
Katika kufanikisha Kongamano hilo Mkurugenzi huyo ameyaomba Mashirika mbalimbali kujitokeza  kufadhili  Kongamano hilo ambalo litakuwa ni msaada mkubwa  wa kuwajenga Vijana hasa mkoani Mara.
 “Mimi nayaomba mashirika mbalimbali kujitokeza ili kufanikisha Kongamano hilo maana najua litakuwa msaada mkubwa sana kwa Vijana ambapo  kwa njia moja au nyingne litaweza kubadili fikra za vijana wanapomaliza masomo yao’ alimalizia Mkurugenzi huyo

Nguvu kazi ya taifa lolote duniani ni vijana,hivyo wasipoandaliwa vizuri leo,kesho watakuwa bomu ambalo litakapolipuka litaangamiza taifa lote.Waafrika wanayo methali isemayo “mtoto umleavyo ndivyo akuavyo”,hivyo kama tunahitaji kuwa na kizazi bora chenye maadili,uzalendo na uwajibikaji tuanze kuwaandaa vijana sasa kisaikolojia,kimaadili na kimtazamo

Afisa Habari na Uhamasishaji
Jamii Information Network

MAZISHI YA SAJUKI YALIVYOKUWA

HIVI NDIVYO MAZISHI YA MPENDWA WETU SAJUKI YALIVYOKUWA - RAISI AUDHURIA

Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akiweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Sajuki wakati wa mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya Kisutu-Dar es Salaam adhuhuri ya leo.
Mwili wa marehemu Sajuki ukipelekwa makaburini.



King Kikii Mwana Fa na Profesa J.

Msanii Z Anto akiswali juu ya kaburi la Marehemu Sajuki.

Hapa ndipo alipozikwa Marehemu Sajuki.
sajuki

Maiti ambayo bado haijafahamika

MAITI YA MTU AMBAYE HAKUWEZA KUFAHAMIKA IMEKUTWA IMEFUKIWA KWA MAWE NA UDONGO HUKO MAKOKO KATIKA MANISPAA YA MUSOMA

KAMANDA WA JESHI LA POLISI MKOANI MARA ABSALOM MWAKYOMA AKIWA NA MWANA HABARI GEORGE MARATO
 
        Na Shomari Binda
              Musoma,

Maiti ya mtu mmoja ambaye hakuweza kufahamika imekutwa imefukiwa kandokando ya miamba ya milima kwa mawe na udongo katika mtaa wa Nyarigamba Kata ya Makoko Manispaa ya Musoma na kuendelea kuwa na hofu kwa Wananchi juu ya mauaji yanayoendelea kutokea katika maeneo mbalimbali katika siku za hivi karibuni.

Katika taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoani Mara ilisema awali kulikuwepo na uvumi  uliohusisha mwili wa marehemu na mwanamke mmoja ambaye amepotea na hajulikani alipo toka tarehe 14.12.2012 katika mazingira ya utatanishi anayeishi katika mtaa wa Ziwani katika kata hiyo ya Makoko.

Taarifa hiyo ilisema baada ya Mwili huo kufanyiwa uchunguzi na madaktari katika hospitali ya Mkoa wa Mara imebainika kuwa mwili huo uliokuwa umefukiwa haujulikani ni wa nani huku ndugu wa Mwanamke aliyepotea wamethibitisha mwili huo sio wa ndugu yao.

"Natoa wito kwa Wananchi wa Musoma na vitongoji vyake pamoja na sehemu nyingine wafike katika Hospitali ya Mkoa wa Mara katika chumba cha kuhifadhia maiti ili kujaribu kuutambua mwili huo ambao umehifadhiwa pale,"alisema Kamanda Mwakyoma.

Mmoja wa shuhuda wa tukio la kufukuliwa kwa mtu huyo Vedastus Masige aliyezungumza na bLOG HII alisema Jeshi la Polisi bado halijaweka nia ya dhati ya kukabiliana na matukio hayo licha kulipotiwa na vyombo vya Habari lakini wamekuwa wakipuuzia huku Wananchi wakiendelea kuangamia.

Alisema hawajasikia Jeshi la Polisi limefikia wapi katika kuchukua hatua juu ya kukabiliana na hali hiyo huku mauaji yakiendelea kutokea na kuwafanya Wananchi wakiishi kwa mashaka na wasiwasi kutokana na hali hiyo inavyoendelea kutokea.

''Tulishuhudia katika siku za nyuma Jeshi la Polisi likihamia Wilayani Serengeti likiongozwa na Kamanda wa Oparesheni wa Jeshi la Polisi Tanzania Chagonja kutokana na kifo cha Mtalii mmoja na waliohusika kukamatwa leo kwa nini wanashindwa kupambana na mauaji yanayokuwa yanatokea mara kwa mara Musoma na Mkoa wa Mara kwa ujumla.

"Haiwezekani kwenye Nchi yetu tuishi kama wakimbizi matukio ya mauaji ya ajabu yamekuwa yakitokea rakini hatua za haraka zimekuwa hazichukuliwi hali ambayo inaendelea kutupa hofu na kuishi kwa mashaka tukiwa katika ardhi yetu inayodaiwa kuwa ni kisima cha Amani,''alisema Vedastus.


Taarifa za kupatikana kwa mwili huo zilitolewa na wavuvi wa dagaa waliokuwa wakianika kwenye jiwe maeneo ya Makoko nje kidogo ya Mji wa Musoma na kusikia harufu ambayo iliwashitua na kuanza kuulizana ni harufu ya kitu gani na inatokea wapi.

"Siku ya kwanza tulisikia harufu lakini tulichukulia ni kawaida lakini muda ulivyozidi kwenda tuliona ikiendelea kuongezeka na kuamua kufatilia kwa kushirikiana na baadhi ya askari wa Jeshi la Wananchi ambao tunaishi nao jirani na kubaini kuna kitu kimefukiwa pembeni ya mlima na kuamua kulitaarifu Jeshi la Polisi,"alisema mmoja wa wavuvi hao aliyekuwa katika eneo la tukio.
Like us on Facebook
Follow us on Twitter
Recommend us on Google Plus
Subscribe me on RSS