Asasi
hii ilianzishwa hapa Musoma kuanzia mwezi Februari mwaka 2011 ikiwa na
wanachama waasisi kumi (10). Wazo la kuanzisha Asasi hii lilitokana na
ukweli kwamba moja ya vikwazo vinavyosababisha kudorora kwa maendeleo
katika jamii za nchi zinazoendelea ni kukosekana kwa taarifa sahihi na
za wakati. Asilimia kubwa ya jamii ya Watanzania wanaishi nje ya miji
ambako kuna uhaba wa vyombo vya kupashana habari kama vile magazeti,
radio, luninga, internet n.k. Kukosekana kwa taarifa za mambo
yanayofanyika ndani ya jamii na nje ya jamii waliyomo kunawanyima fursa
ya kushiriki katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za kijamii,
kiuchumi na kiutamaduni ili kwenda na mabadiliko katika dunia ya leo ya
sayansi, tekinolojia na utandawazi.
DIRA
Kuwa
na jamii yenye uelewa mpana wa habari sahihi za masuala ya kijamii,
kiuchumi na kiutamaduni na kutambua mabadiliko yanayotokea kati yake na
jamii zingine ili kukabiliana na changamoto za kimaendeleo.
DHAMIRA
Asasi
inadhamiria kushiriki na kushirikisha ngazi zote za kijamii hasa
makundi yaliyoko pembezoni katika ukusanyaji, uandikaji, usambazaji na
upashanaji habari.
MADHUMUNI
Kuhabarisha jamii jinsi ya kukabiliana na changamoto za athari na madhara umasikini,
Rushwa na VVU/UKIMWI.
Kushirikisha jamii katika ukusanyaji wa taarifa muhimu, kuziandika na kuzisambaza ili
Kuimarisha mawasiliano ya habari.
Kuimarisha mitandao ya mawasiliano ndani ya jamii ili jamii iweze kupata taarifa sahihi
Zinazoendana na wakati.
Kushirikisha jamii katika kuibua changamoto na kukuza ushawishi na utetezi wa sera
Mbalimbali kwa njia ya midaharo ili ziwe na tija kwa jamii.
Kufanya tafiti mbalimbali za masuala ya kijamii, kiuchumi na kiutamaduni ili kuzipatia
Ufumbuzi.
Kuyajengea uwezo makundi mbalimbali ya kijamii Kwa njia ya vipeperushi, magazeti,
Radio, TV na mafunzo ili kupata ufahamu wa kujiletea mabadiliko.
Kukuza uelewa wa jamii juu ya kutambua na kutetea haki zao za msingi zinazokiuka Misingi ya demokrasia, usawa, utawala bora, uwazi na uwajibikaji.