UKATILI HUU MPAKA LINI: TAZAMA ALBINO HUYU ALIVYO KATWA MKONO NA KUJERUHIWA VIBAYA, SHUHUDIA
Posted by jamii information network
Posted on Sunday, May 26, 2013
HAKI ZA WANAWAKE MNAYAONA HAYA?: MWANAMKE AFUNGWA MNYORORO KATIKA MTI NA MUMEWAKE ILI ASITEMBEE. SHUHUDIA
Posted by jamii information network
Posted on Sunday, May 26, 2013
Mtandao huu ukakuta unyanyasaji wa namna hii bianadamu anafungwa minyororo kama mtumwa .Huu nao ni ukatili kupindukia tupendane kama watoto wa mama na baba mmoja.
KWA UNYAMA HUU SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE
Posted by jamii information network
Posted on Friday, May 17, 2013
Taasisi ya Jamii Informatio Network inayojihusisha na Uhamasishaji wa Maendeleo na Mawasiliano unatoa pole kwa Familia ya Mtoto huyu lakini pia inaomba vyombo vya dola kuhakikisha sheria inachukua Mkondo wake
TAMKO LA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU DHINI YA AGENDA ZA KUVURUGA AMANI YA NCHI NA VITISHO KWA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU NCHINI
Posted by jamii information network
Posted on Sunday, May 12, 2013
Watetezi kutoka mikoani ambao ni wanachama wa Mtandao wa
Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini (THRD-Coalition), waliokutana kwa siku tatu
jijini Dar es Salaam, pamoja na kupata mafunzo adhimu ya usalama kwa watetezi yatolewayo na
THRD-Coalition, pia walifanya tathmini ya hali ya usalama kwa watetezi nchini; asasi za haki za binadamu, waandishi wa habari
na watu wanaojitolea katika eneo la msaada wa kutetea wenzao yaani
(volunteers). Tathmini imeonyesha kwamba yapo mambo kadhaa yanayosababisha
kukosekana kwa usalama kwa watetezi nchini na kupotea kwa amani.
1. Utendaji wa Vyomba Serikali na Vuguvugu la Kisiasa
Serikali ndicho chombo chenye jukumu la kuwalinda watetezi wa
haki za binadamu na watu wengine waliomo ndani ya mipaka ya nchi yetu, wao na
mali zao. Vitendo vya watu kujichukulia sheria mikononi mwao, kuteka, kutesa,
kung’oa meno, na macho, kukata vidole na hata kuwarushia bomu waamini wakiwa
katika maeneo ya maombi ni ishara ya dhahiri ya serikali iliyoshindwa kutimiza
majukumu yake. Vitendo vya baadhi ya viongozi nchini hasa katika ngazi za
Serikali za Mitaa kuwakandamiza watetezi wa haki za binadamu kwa namna
mbalimbali ikiwemo kuwafungulia kesi za kubambikiza vimefikia kiwango cha
kutovumilika. Matamko mengi yanayotolewa na viongozi wa juu wakiwamo mawaziri
dhidi ya watetezi na asasi za haki za binadamu nchini yanaonyesha kuwa ni
viashiria vya vitisho vya kiusalama wazi wazi kwa watetezi nchini. Pia watetezi
wamekuwa wakishutumiwa kuwa ni wapinzani kwa sababu kazi zao zimekuwa
zikilinganishwa na kazi za vyama vya upinzani na za kiuchochezi.
Kuwa mtetezi ni kiungo
muhimu katika kuibua na kufichua maovu ili kujenga utawala unaoheshimu haki za
binadamu, lakini siku zote tumejikuta tukihatarisha maisha yetu. Katika
mazingira ya aina hiyo watetezi hawawezi kujiweka katika kundi salama hata
kidogo, bali kwamba usalama wao umo hatarini kwa sababu kazi nyingi
wanazozifanya huwalazimisha kuikosoa serikali pale inapokuwa haitimizi wajibu
wake kuhusiana na kulinda haki za msingi za binadamu na haki nyinginezo stahiki.
Mifano halisi ya migongano kati ya asasi
na serikali ni kesi za kugombea ardhi Pugu, Loliondo, Bagamoyo na migogoro
isiyoisha katika migodi mkoani Mara.
2. Wamiliki wa vyombo vya habari
Katika
kudadisi ni kwa nini wanahabari wanakabiliwa na changamoto nyingi za kiusalama
iligundulika kwamba wamiliki wa vyombo hawana mikakati mizuri juu ya suala zima
la usalama kwa waandishi wao. Pia malipo finyu kwa wanahabari ilionekana kuchangia kwa kiasi kikubwa kwa sababu baadhi
yao hawapati malipo ya uhakika wala mikataba. Hali hiyo husababisha waandishi
waishi maisha ya kubahatisha na wakati mwingine hujikuta wakishawishika kuingia
katika makundi ya kisiasa ili kuanza
kuvitumikia ‘vyanzo vyao’ jambo ambalo husababisha wakiuke maadili ya kazi zao
na mwisho hushambuliwa na wale wanaoguswa na habari za aina hiyo. Aidha
watetezi wanawasihi wamiliki kuanza kuweka mikakati ya kiusalama kwa waandishi
na kuboresha mishahara kwa waandishi ili wafanye kazi kwa uhakika zaidi.
3. Jeshi la Polisi
Jeshi la
Polisi wawe makini na matumizi ya silaha za moto na nguvu za ziada ambazo
zimekuwa zikisababisha vifo na ulemavu wa kudumu. Katika purukashani nyingi za
kisiasa jeshi hilo limeshindwa kabisa kuonyesha kwamba linafanya kazi ya
kuutumia umma wa Watanzania wote na badala yake limekuwa likichukua mwelekeo wa
kuwatumikia wanasiasa au chama fulani. Aidha askari polisi wanakumbushwa kwamba wao ni sehemu ya jamii
na hao wanaowatesa ni ndugu zao wa karibu wadogo zao mama zao n.k. Jeshi la
Polisi litambue kuwa kazi za watetezi wa haki za binadamu ni kazi halali
zinazolindwa kisheria na wanajukumu la kuweka mazingira mazuri ya watetezi
kufanya kazi zao bila kutekwa, kuteswa ama kungo’lewa macho, meno, kucha n.k. Mfano halisi wa mapungufu ya
jeshi hilo ni kukamatwa kwa askari hivi karibuni waliokuwa na fuvu la kichwa
cha mtu mkoani Morogoro kwa lengo la kumbambika mtu kesi ya jinai. Tunaisihi
Serikali na Jeshi la Polisi kuanza kutekeleza Tamko la Umoja wa Mataifa la
tarehe 15 Machi 2013 linalotaka mataifa yote kutambua umuhimu na uhalali wa
majukumu ya watetezi wa haki za binadamu katika kutetea haki za binadamu
demokrasia, utawala wa sheria, kama nyenzo la kuhakikisha usalama wao ikiwa ni
pamoja na kuheshimu uhuru wa asasi zao na kuepuka kunyanyapaa shughuli za asasi
za kiraia.
4. Wanaharakati na Watetezi wa Haki za Binadamu
Wanaharakati
wote na watetezi wa haki za binadamu wasichukue upande wowote katika masuala ya
itikadi za kisiasa kwani wao ni watu wa kati. Pia wanaharakati wasijiingize
katika matumizi ya nguvu au kupambana na Jeshi la Polisi. Aidha wanaharakati
wametakiwa kuwa waelimishaji wa umma na kujizuia kujiingiza katika mambo
yaliyopandikizwa na watu wasioitakia mema nchi yetu kama vile udini na migogoro
isiyoisha ya kugombea ardhi, maeneo ya malisho, ukabila n.k.
5. Vurugu za Udini
Kwa miaka
mingi Tanzania haikuwahi kupata misukosuko ya udini kama inayotokea sasa.
Lakini kwa miaka ya hivi karibuni uhasama wa kidini umezidi kushamiri. Watetezi
kwa umoja wetu tunaamini Tanzania hatuna udini bali kinachoendelea ni ajenda za
watu fulani kwa maslahi binafsi ama ya kifedha, kidini au kisiasa. Kwa sasa
nchi inaweza kutumbukia katika machafuko ya kidini endapo viongozi wa dini
zote, wanasiasa na serikali hawatachukua hatua za makusudi kuwakomesha wachache
hao ambao wanataka kuondoa amani ya nchi. Katika mazingira haya pia mtetezi wa
haki za binadamu hawezi kubakia salama
na ndio maana tunakemea kwa nguvu zote vitendo hivi viovu.
6. Watanzania Wote Kwa Ujumla
Watanzania katika ujumla wao wameaswa kuwa makini hususani wakati huu tunapoelekea katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Wapo watu wanaochomekea ajenda zao kwa malengo wanaoyafahamu wao wenyewe na hivyo kuligawa taifa katika misingi ya udini na mambo mengine kama hayo yasiyo na tija wala manufaa kwa nchi yetu. Aidha Watanzania wameshauriwa kuirejea kazi nzuri ya kuwaunganisha ambayo iliifanya nchi hii ifahamike kama kisiwa cha amani miongoni mwa Jumuiya ya Kimataifa.
Mwisho
tunaungana na watanzania wengine kulaani kitendo cha kutupa mabomu katika
mikusanyiko ya watu kama ilivyotekea kule Arusha. Tunawapa pole wafiwa na majeruhi
wote. Na kutaka watanzania wote bila kujadili itikadi zao kuendelea kulaani
vitendo hivi vya kinyama.
TAMKO HILI LIMEANDALIWA NA WATETEZI 30 WA HAKI ZA BINADAMU TOKA MIKOA MBALIMBALI
KWA NIABA YA WENZAO KATIKA AZIMIO LA KUIREJESHA NCHI HII KATIKA HALI YA AMANI
NA UTULIVU
KWA PAMOJA TUTAFANIKIWA TUNAOMBA MSAADA WAKO.
Posted by jamii information network
Posted on Friday, May 10, 2013
Taasisi ya kuhamasisha maendeleo na
mawasiliano katika jamii yenye makao yake mjini Musoma mkoani Mara ya JAMII INFORMATION NETWORK inatarajia
kufanya Kongamano kubwa litakalo wahusisha Wanafunzi zaidi ya 200 kutoka Shule 10 za
Sekondari za Manispaa ya Musoma Mwezi August Mwaka huu, ikiwa ni njia ya kuhamasisha Maendeleo na kuimarishaji wa Mawasiliano
ndani ya Jamii.
Katika
Kongamano hilo mada mbalimbali zitatolewa na Wataalamu waliobobea katika Masuala
uhamasishaji wa Vijana Kupambana dhidi ya Ukimwi,ujasiriamali,dhana ya
kujiajiri,Changamoto katika Elimu kwa Vijana
pamoja na Ukatili wa Kijinsia ikiwa ni njia ya kujenga Msingi bora wa
Makuzi kwa Vijana wetu.
Mbali
na hivyo vijana hao pia wataelezwa jinsi ya kuwa Wazalendo katika nchi
yao,kupambana na rushwa,Umaskini lakini pia wakipata elimu sahihi ya faida za
uwekezaji kwa Tanzania,Sababu za Mimba za Mapema kwa watoto wa kike na jinsi ya
kujenga Mahusiano na Mawasiliano yaliyo sahihi.
Pamoja
na Mtandao huu kuwa na nia njema katika kuwasaidia Vijana lakini bado
kumekuwepo na Changamoto mbalimbali katika kufanikisha Kongamano hilo hasa
katika Suala la kifedha,hivyo basi Taasisi ya JAMII INFORMATION NETWORK kwa nia njema inakuomba wewe
Mtanzania,Mpenda Maendeleo,unaekaa ndani au nje ya nchi,Mashirika kusaidia Taasisi
hii katika kufanikisha Kongamano hilo ili vijana wetu wakue katika Makuzi mema
na kujenga Tanzania ya kesho
iliyostaarabika.
Blog Master
ASKARI ALIYEUA TARIME CHINI YA ULINZI
Posted by jamii information network
Posted on Friday, May 10, 2013
Mwanafunzi
mmoja wa darasa la kwanza katika shule ya msingi rebu wilayani tarime mkoani
mara deus jacob,ameuawa kinyama baada ya kupigwa risasi kichwani na askari
polisi wa wilayani tarime wakati
wakiwa katika harakati za kumkamata
mtuhumiwa wa kosa la kushambulia na kujeruhi.
kamanda wa
polisi kanda maalum ya tarime rorya,kamishina msaidizi justus kamugisha,amesema mwanafunzi huyo mkazi
wa songambele wilayani tarime amepigwa risasi hiyo ambayo imesababisha kupoteza
maisha na askari polisi mwenye namba d 4662 koplo methew wakati akipita barabarani.
kamanda
kamugisha amesema kuwa risasi hiyo ambayo imemuawa mwanafunzi huyo ni miongoni
mwa risasi tano ambazo zilifyatuka wakati wa porukushani ikihusisha mtuhumiwa huyo marwa chacha na askari polisi katika jaribio la kupora bunduki.
kwa mujibu
wa kamanda kamugisha askari polisi huyo
anashikiriwa kwa mahojiano wakati wakimtafuta mtuhumiwa marw chacha ambaye alikimbia baada ya tukio hilo
kutokea ambapo polisi walifanikiwsa
kukamata misokoto ya bangi 45 na kilo 3 na roba za bangi kavu ambayo inadaiwa
ni mali ya mtuhumiwa huyo.
kwa upande
wake mzazi wa mwanafunzi huyo mzee jacob mwita sasi,amelaani kitendo cha polisi
huyo kumua mtoto wake kwa risasi bila kosa hivyo kutaka vyombo vya sheria
kuchukua harua ili kuhakikisha haki inatendeka.
MUHIMU KWA WADAU WA BLOG HII! NDANI NA NJE YA NCHI
Posted by jamii information network
Posted on Friday, May 10, 2013
Mpendwa Msomaji wa blog hii ya JAMII INFORMATION NETWORK
tunashukuru sana kwa kuitembelea Blog hii ambayo ni blog inayomilikiwa na Taasisi ya JAMII INFORMATION
NETWORK (JIN) inayojihusisha na
Uhamasishaji wa Maendeleo na Mawasiliano katika Jamii.
Blog hii
itakuwa ikikueleza matukio mbalimbali ya Kijamii ambayo yatakuwa yanaigusa
Jamii moja kwa moja au kwa njia nyingene na pia kuibua changamoto zilizopo katika
Jamaii yetu,Hivyo basi tunaomba utuunge Mkono katika kuitazama blog hii.
Blog Editor
POLISI WAUA TARIME MTOTO WA MIAKA 9 KWA RISASI
Posted by jamii information network
Posted on Thursday, May 09, 2013
Haya ndiyo yaliyofanyika Tarime leo mtoto wa miaka 9 kuuuwa na jeshi la polisi kwa uzembe eti wanawakamata majambazi ambao si wale wanaoiba na kuuwa watu mpaka mwa Tanzania na Kenya kashuhudie mwenyewe uone then comment! hATA HIVYO UNAOWAONA NI WANANCHI WALIOCHOKA WAKIANADAMANA HUKU WAMEBEBA KWENYE MACHELA MWILI WA MAREHE dEO yKOB MWNAFUNZI WA DARASA LA TATU KATIKA SHULE YA MSINGI MTURU MJINI HAPA! Nimelishuhudia hili.
MLEMAVU WA NGOZI (ALBINO) ASIMAMISHWA SHULE KWA KUTUHUMIWA KUWA MSHIRIKINA MLOWO MBOZI
Posted by jamii information network
Posted on Thursday, May 09, 2013
Hapa Amina akimsimulia mkasa mzima mwandishi wa Mbeya yetu Joseph
Mwaisango mara baada ya kupata maelezo yote ya Amina mwandishi wetu
alimpigia simu katibu wa chama cha maalbino mkoa wa Mbeya afike ofisi ya
Mbeya yetu ili wasaidiane kutatua tatizo hilo
katibu wa Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya, Wiliamu Simwale alifika ofisi ya Mbeya yetu na kuanza kumsikiliza Amina
katibu wa Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya, Wiliamu Simwale akiwa makini kumsikiliza Amina katika ofisi ya Mbeya yetu
KATIKA Hali isiyokuwa ya Kawaida Uongozi wa Shule ya Sekondari Hollwood iliyoko Mlowo Wilayani Mbozi Mkoa wa Mbeya imemsimamisha shule Mwanafunzi wa kidato cha tatu kwa takribani Miezi Miwili kwa madai kuwa anajihusisha na imani za Kishirikina.
Mwanafunzi huyo aliyejulikana kwa jina la Amina Mwankinga(20) ambaye ni mlemavu wa ngozi(Albino) alisimamishwa shule na uongozi wa Shule hiyo tangu Machi 9, Mwaka huu baada ya uongozi wa Shule hiyo kupata taarifa kutoka kwa Wanafunzi wakimtuhumu Mwenzao huyo kuwa ni Mshirikina.
Uongozi wa Shule hiyo baada ya kupata taarifa hizo ulimwamuru mhanga wa tukio hilo kuondoka Shuleni hapo pasipo kufuatilia na kujua ukweli wa jambo hilo na kupata udhibiti hivyo kumwacha Mwanafunzi huyo akizurura mitaani asijue hatma ya maisha yake.
Mhanga wa tukio hilo Amina Mwankinga alisema tangu tarehe tisa alipofukuzwa bwenini na wanafunzi wenzie wakitaka aondoke shuleni hapo majira ya usiku hali iliyomlazimu kuomba hifadhi kwa mlinzi aliyemkubalia na kukesha naye hadi asubuhi hali iliyopelekea kupigwa na baridi kali kutokana na kukosa nguo za kujisitiri kama Shuka nk.
Anasema kutokana na hali hiyo Walimu pamoja na uongozi wa Shule hiyo haukuchukua hatua yoyote jambo lililomlazimu kuondoka Shuleni hapo baada ya kukosa msaada ambapo alirejea Jijini Mbeya anakoishi na Binamu yake.
Binti huyo anayesomeshwa na Shirika la Under the SameSun iliyoko Jijini Dar Es Salaam aliwaambia waandishi wa habari kuhusu mkasa uliompata huku akiomba msaada kwa wasamaria wema kumtafutia Shule ili aendelee na masomo kwa ajili ya kujiandaa na mtihani wa kidato cha nne Mwakani.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya HollyWood Ambukeghe Mtafya, alipopigiwa simu kuhusu tuhumahizo alikiri kulijua suala hilo na kwamba walimrudisha mwanafunzi huyo nyumbani ili kumnusuru na kipigo kutoka kwa wanafunzi wenzie na kuongeza kuwa aliambiwa atafute shule nyingine ili ahamie.
Naye katibu wa Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya, Wiliamu Simwale alisema alikuwa halijui suala hilo na kwamba kama lingekuwa suala liko nyeti angejulishwa yeye juu ya hatua zilizofikiwa ambapo Uongozi wa Shule umeendelea kupokea fedha za malipo ya Mwanafunzi pasipo kutoa taarifa kwenye shirika linalolipa.
Mlezi wa Wanafunzi hao kutoka Shirika la Under the Samesun Omary Mfaume amesema kwamba hana taarifa zozote kuhusiana na tukio hilo na kuongeza kuwa anawasiliana na uongozi wa Shule moja kwa moja ili umweleze juu ya kilichotokea ili taratibu za kumtafutia Shule nyingine zifanyika haraka ili Mwanafunzi aendelee na masomo kama kawaida.
Source Mbeya yetu
Shirika la Save the Children, limeeleza kuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuwa ndio nchi ngumu zaidi duniani kulea watoto.
Posted by jamii information network
Posted on Thursday, May 09, 2013
Wanawake DRC
wakiandamana.
|
Shirika la
Save the Children, limeeleza kuwa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuwa
ndio nchi ngumu zaidi duniani kulea watoto.
Nchi ya
Finland imetajwa kuwa sehemu bora duniani kuwa mama, huku Sweden na Norway
zikifuatia katika nafasi ya pili na tatu.
Shirika hilo
la hisani limetumia vigezo vya huduma ya afya kwa akina mama, vifo vya watoto,
elimu na kipato katika nchi 186 duniani kutoa takwimu hizo.
Nchini
India, zaidi ya watoto 300,000 hufariki dunia saa 24 baada ya kuzaliwa, hivyo
kuchangia 29% ya vifo vya watoto wanaozaliwa duniani kote, imeeleza ripoti ya
shirika hilo.
Nchi kumi
zilizoshika nafasi ya mwisho zote zinatoka eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara,
ambako kwa wastani, mwanamke mmoja katika 30 hufariki dunia kutokana na
matatizo ya ujauzito na mtoto mmoja kati ya saba hufariki kabla ama baada ya
kufikisha umri wa miaka mitano.
Nchini DRC,
vita na umasikini vimewaacha akina mama wakiwa dhoofu kiafya na bila msaada
wowote hasa wakati wa hatari kubwa katika maisha yao.
Nchi
nyingine zilizotajwa kuwa hatari ni Somalia, Sierra Leone, mali, Niger, Jamhuri
ya Afrika ya Kati, Gambia, Nigeria, Chad na Cote D’Ivoire.
Congo
ni mahali hatari zaidi kwa
akina
mama
|
Shirika hilo
la hisani limesema, ukosefu wa lishe bora ni sababu kubwa ya kuongezeka kwa
idadi ya vifo vya akina mama na watoto wachanga katika nchi za Kusini mwa
Jangwa la Sahara, huku 10% - 20% ya akina mama wakiwa hawana uzito unaostahili.
Kinyume
chake, matokeo hayo yanaonesha kuwa, Finland ni nchi bora kuwa mama, huku
hatari za vifo vitokanavyo na ujauzito ikiwa ni moja kati ya akina mama 12,200
na watoto katika nchi hiyo wakihudhuria karibu miaka yote 17 ya elimu ya awali.
Sweden,
Norway, Iceland na Uholanzi zilikuwa pia miongoni mwa nchi bora 10, ambapo
Marekani iko nyuma katika nafasi ya 30.
Lakini jambo
la kustaajabisha, ripoti ya shirika hilo imebaini kuwa, Marekani ina kiwango
cha juu cha vifo vya watoto wanaozaliwa katika nchi zenye viwanda duniani,
ambapo watoto 11,300 hufariki dunia katika siku wanayozaliwa kila mwaka.
Shirika hilo
limesema, hali hiyo inasababishwa na idadi kubwa ya watu nchini Marekani pamoja
na wingi wa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati.
Marekani ni
miongoni mwa nchi zenye kiwango cha juu cha watoto wanaozaliwa kabla ya wakati
ikiwa na uwiano wa mtoto mmoja kati ya wanane.
Ripoti hiyo
imegundua kuwa, akina mama na watoto hufariki dunia kwa idadi kubwa huko Kusini
mwa Asia kuliko eneo lolote duniani, ikikadiriwa kuwa, watoto 423,000 hufariki
dunia siku wanayozaliwa kila mwaka.
India
imetajwa kuwa na idadi kubwa ya vifo vya watoto wachanga,(ikiwa ni 29% ya vifo
duniani) na pia vifo vingi vya akina mama kuliko nchi yoyote duniani ambapo
akina mama 56,000 hufariki kila mwaka.
Chanzo:BBC.
WANAHABARI NCHINI WAASWA KUANDIKA HABARI ZINAZOKIUKA HAKI ZA BINADAMU
Posted by jamii information network
Posted on Thursday, May 09, 2013
Vick Ntetema akitoa somo
Malima Lubasha
Picha ya Pamoja
Stephen Wang'anyi akiwa na Vick Ntetema
Augustine Mgendi akiwa pamoja na Vick Ntetema
Anthony Mayunga Katika harakati
Mtoto ambaye naye hakuwa nyuma katika kupata elimu ya utetezi wa haki za binadamu
Mratibu wa THRD -Coalition Onesmo Olengurumwa
Wadau wa utetezi wa haki za Binadamu
Anthony Mayunga akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Under the same Sun Vick Ntetema
Waandishi wa habari nchini
waaswa kuandika habari za utetezi wa haki za Binadamu,Kauli hiyo imetolewa na
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Under The Same Sun Vick Ntetema
wakati akifungua Mafunzo ya Usalama na Tathimini ya Athari kwa Wanachama wapya wa Shirika laa Tanzania
Human Rights Defender Coalition (THRD-Coalition).
Amesema kumekuwepo na Matukio mengi ya Unyanyasaji na
Ukiukwaji wa haki za Binadamu hivyo basi Waandishi wa habari wanapaswa kutumia
kalamu zao katika kuibua Ukiukwaji Mkubwa wa haki za Binadamu unaofanywa hapa
nchini.
Kwa Upande wake Onesmo Olengurumwa alisema kuwa Mafunzo hayo kwa waandishi wa habari
yatasaidia Mwanahabari kufanya kazi katika Mazingira salama kutokana na Vitendo
vilivyoshamiri hivi sasa vya kuwateka Wanahabari.
Alisema Mwanahabri anapaswa kufanya kazi yake katika
Mazingira ambayo yatamfanyaa awe salama Siku zote hivyo basi Mafunzo hayo
yatatoa Mwanga kwa wanahabri katika utetezi lakini pia wanahabri kufanyakazi
wakiwa katika Mazingira Salama.