Karibu Musoma Information Center kwa huduma zifuatazo:- 1) Kwa kutengenezewa design mbalimbali kama za Business card, Vipeperushi, mabango mbalimbali, kadi za Harusi za kisasa zaidi, kadi za mialiko mbalimbali, Vitambulisho vya wanafunzi wa sekondari na katika kampuni mbalimbali ( ID cards) na kadi nyinginezo zenye design ya kuvutia. 2) Kutengenezewa mabango ( Posters) mbalimbali zinazohusu biashara ya mhusika au bidhaa mbalimbali. 3) Kutengenezewa nembo ( LOGO) za kuhusiana kampuni au biashara yako. 4) Tunatengeneza tovuti ( Websites ) zenye kiwango ambacho huwezi amini kama zinatengenezwa musoma, kwa bei nafuu ambayo huwezi ipata kwingine isipo kuwa kwetu. 5) Mwisho tunatoa ushauri na elimu kuhusiana na maswala ya computer.5) Sisi ni watengenezaji wa blog zinazokaa mfumo wa website. kama hii unayoiona.

TUSHIRIKIANE KATIKA KUPAMBANA NA VITENDO HIVI VYA KIKATILI


 
Na Waitara Meng’anyi, Tarime
 
Ghati Chacha (21) mkazi wa kijiji cha Nyanitira kata ya Nyansincha Wilayani Tarime amesababishiwa kilema cha maisha kwa kukatwa mguu wake wa kulia na Mume wake baada ya kuchelewa kumfungua mlangao nyakati za usiku.
 
Akisimulua mkasa huo hivi karibuni akiwa wodi  namba sita alikolazwa akiuuguza vidonda na majeraha,Ghati alisema, mume wake  aliye mtaja kwa majina ya Chacha Mwita(23) alifika nyumbani saa mbili usiku akiwa amelewa.
 
“Aliniuliza kwa nini nimechelewa kumfungulia mlango nikamjibu sikuwa nasikia, baadaye akaniomba kurunzi na panga, nikamletea kurunzi na kumwonesha panga lilipo  kwa kidole” alisema Ghati.
 
Wakati anamwonesa lilipo panga na kumpa kurunzi Ghati hakujuwa kuwa nini kinafuata  alifiki kuwa mambo ya wanaume pengine anataka kwenda  sehemu kwa kuwa ndizo tabia za wanaume wa maeneo haya kuondoka usiku ama anataka kuangalia mji kama uko sawa alafu arudi kulala.
 
“ Alipoipata ile panga akaniambia leo atamitumbua utumbo, akaanza kunipiga kwa  panga ile akanijeruhi sikio, mkono wa kushoto na mguu wa kushoto na kunikata mguu wa kulia  ukakatika kama unavyoona” alieleza kwa masikitiko akiifunua kanga iliyokuwa amejifunika akiwa amelala kitandani  hospitali ya Wilaya Tarime.
 
Wakati anafanyiwa ukatili huo ali piga kelele lakini majirani hawakuwahi kufika  kumsaidia kwa kuwa ni kawaida ya mume na mke kugombana na vilio kama hivyo kusikika katika maeneo hayo.
“Baadaye walikuja na aliposikia majirani wamefika alikimbia kwa kupitia mlango wa nyuma akitumia baisikeli yake, majirani walinifunga mguu uliokuwa ukivuja damu na kunikimbiza katika kituo cha afya Muriba na baadaye kuletwa hapa” alieleza .
 
Hata hivyo mwanzoni Ghati alieleza kuwa chanzo cha matatizo hayo yote ni ndoa za mitala na unywaji wa pombe wa mume wake.
 
“ Nimeishi naye kwa miaka mine sasa na tuna watoto wawili na tulikuwa tunaishi vizuri, tatizo akinywa pombe huonekana kama amewehuka linguine ni  baada ya kuoa mke wa pili ambapo alianza kunichukia , kuanza kunipiga na sasa kunikata mguu” alisema Ghati.
 
 Ghati hataweza kurudiana na mume wake huyo  kwa kitendo alichomfanyia kwa vile amesema hakioneshi utu na kuiomba mahakama imuhukumu mumewe kifungo jera ili  ajifunze kutokana ukatili aliomfanyia.
 
” Naomba serikali na watu binafsi wanisaidie magongo ya kutembelea kwa kuwa sasa sina uwezo wa kuyanunua pia wanisaidie kusomesha watoto wangu maana ni wadogo na mimi ndiye niliye kuwa nikitafuta tunakula” alisema.
Wananchi walioshuhudia kitendo hicho walionesha kusikitishwa  na kukilaa kuwa kinaendelea kuharibu jina la na sifa ya Wilaya ya Tarime .
 
“ Sikifurahii kitendo hiki kwani kinaonesha wazi ukatili wa hali ya juu kwa binadamu mwenzako  na hii inasababisha hata watu ambao hawajawahi kufika huku  kutuona  sisi  ni wanyama kumbe ni watu wachache wanaotuharibia sifa, mahakama imuhukumu huyu mtu  adhabu kubwa inayomstahili ili liwe fundisho kwa wengine” alisema Mwita Machera aliyekuwa  hostalini hapo.
 
Jeshi la polisi baada ya kupata taarifa lilifika lilifika eneo hilo la tukio na kushuhudia kipande cha mguu kama inavyoonekana kwenye picha hapa na kuamru kizikwe na juhudi za kumtia nguvuni kuanza.
 
Hata hivyo siku mojs baadaye Chacha Mwita alikamatwa na jeshi la polisi kwa kusaidiana na nguvu nza wananchi ambapo alifikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Tarime kujibu mashitaka hayo.
 
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamishina masaidizi wa polisi kanda maalumu ya Tarime (ACP) Justus Kamugisha lisema kuwa baada ya kuhojiwa Mwiata alikiri kumsababishia mke wake ukilema wa maisha.
 
“ Vitendo vya kikatili vilishapitwa na wakati, kumsababishia mtu ukilema wa maisha sii jambo lisilo la utu na linaonesha kuwa hakuna ubinadamu kwa watu  japo si wote” alisema Kamugisha kwa nija ya simu.

NI JUKUMU LETU KUWASAIDIA VIJANA KATIKA KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA

IKIWA Tanzania leo inaungana na ulimwengu mzima kuazimisha siku ya kupinga matumizi ya dawa za kulevya,jamii hususani vijana wametakiwa kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya mbayo yamekuwa yakiathiri nguvu kazi ya Taifa na kuwafanya vijana wengi kuishi katika hali hatalishi.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Shirika la Jamii Information Network linaloshughulika na utoaji elimu katika utambuzi wa mambo mbalimbali yenye kujenga jamii Augustine Mgendi alipokuwa akizungumza na Blog hii namna vijana wengi walivyoathirika kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya.

Amesema vijana wengi ambao ndio tegemeo katika ujenzi wa Taifa wamejitumbukiza katika matumizi ya dawa za kulevya na hivyo kushindwa kushiriki ipasavyo katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo huku wengi wao dawa hizo zikiwatuma kushiriki katika vitendo vya uhalifu.

Mgendi amedai ikiwa Tanzania inaungana na mataifa mengine Duniani katika kupinga matumizi ya dawa za kulevya pia inawajibu ya kupanga mikakati kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali katika kutoa elimu katika sehemu mbalimbali juu ya athari kubwa zinazotokana na dawa za kulevya ili kila jamii hasa vijana waweze kuepukana na matumizi yake.

Amesema wapo vijana ambao wanajiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya bila kufahamu athari zake na wengine kwa kuiga wale wanaotumia hali ambayo inafanya kuongezeka kwa idadi kubwa ya vijana wanaojiingiza katika matumizi ya dawa hizo.
Akitolea mfano wa dawa za kulevya aina ya bangi (Cannabis) kitaalam inamfanya mtumiaji kukosa umakini na kushindwa kufanya vitu vinavyohitajika na uwezekano mkubwa kupata kansa na kuharibu mapafu kutokana na matumizi ya muda mrefu na hata kupelekea kuzaa vilema.

"Zipo athari nyingi kutokana na matumizi ya dawa za kulevya aina ya bangi ambayo vijana wengine wamejitumbikiza huko,lakini wapo wengine kutokana matumizi ya bangi kunawapelekea kuchanganyikiwa na kupumbaa kwa ufahamu hivyo kunahitajika elimu.
"Licha ya bangi,dawa za kulevya aina ya (Narcoticks) ambapo ndani yake kuna dawa kama Heroine,darvon,hydrocodone,codeine vijana ujiingiza kuzitumia bila kujua athari zake na pengine bila kupata elimu hivyo kuendelea kuangamiza Taifa.

"Moja ya athari ya dawa hizi ni kupoteza fahamu,kuugua ugonjwa wa kifafa na hata kifo pale utakaozidisha kipimo,sasa kama elimu haitatolewa kwa vijana kwa kuzitambua athari zake  tutapoteza vizazi vingi,"alisema Mgendi.

Amesema kutokana na gharama kubwa ambazo hutumika kurudisha hali ya kawaida ya mtumiaji wa dawa za kulevya,Shirika la Jamii Information Network kwa 
kushirikiana na wadau wa Mashirika mengine ya kijamii wamekusudia kutoa elimu ili kuweza kuwaepusha vijana na kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya ambapo wameanda Kongamano kwa vijana mwezi August mwaka huu katika kutoa elimu kwa zaidi ya Vijana 200 wa Manispaa ya Musoma

UKATILI HUU MPAKA LINI: TAZAMA ALBINO HUYU ALIVYO KATWA MKONO NA KUJERUHIWA VIBAYA, SHUHUDIA

HAKI ZA WANAWAKE MNAYAONA HAYA?: MWANAMKE AFUNGWA MNYORORO KATIKA MTI NA MUMEWAKE ILI ASITEMBEE. SHUHUDIA


Mtandao huu ukakuta unyanyasaji wa namna hii bianadamu anafungwa minyororo kama mtumwa .Huu nao ni ukatili kupindukia tupendane kama watoto wa mama na baba mmoja.

KWA UNYAMA HUU SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE


Taasisi ya Jamii Informatio Network inayojihusisha na Uhamasishaji wa Maendeleo na Mawasiliano unatoa pole kwa Familia ya Mtoto huyu lakini pia inaomba vyombo vya dola kuhakikisha sheria inachukua Mkondo wake

TAMKO LA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU DHINI YA AGENDA ZA KUVURUGA AMANI YA NCHI NA VITISHO KWA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU NCHINI




                                                           
Watetezi kutoka mikoani ambao ni wanachama wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini (THRD-Coalition), waliokutana kwa siku tatu jijini Dar es Salaam, pamoja na kupata mafunzo  adhimu ya usalama kwa watetezi yatolewayo na THRD-Coalition, pia walifanya tathmini ya hali ya usalama kwa watetezi nchini;  asasi za haki za binadamu, waandishi wa habari na watu wanaojitolea katika eneo la msaada wa kutetea wenzao yaani (volunteers). Tathmini imeonyesha kwamba yapo mambo kadhaa yanayosababisha kukosekana kwa usalama kwa watetezi nchini na kupotea kwa amani.

1.      Utendaji wa Vyomba Serikali na Vuguvugu la Kisiasa

Serikali ndicho chombo chenye jukumu la kuwalinda watetezi wa haki za binadamu na watu wengine waliomo ndani ya mipaka ya nchi yetu, wao na mali zao. Vitendo vya watu kujichukulia sheria mikononi mwao, kuteka, kutesa, kung’oa meno, na macho, kukata vidole na hata kuwarushia bomu waamini wakiwa katika maeneo ya maombi ni ishara ya dhahiri ya serikali iliyoshindwa kutimiza majukumu yake. Vitendo vya baadhi ya viongozi nchini hasa katika ngazi za Serikali za Mitaa kuwakandamiza watetezi wa haki za binadamu kwa namna mbalimbali ikiwemo kuwafungulia kesi za kubambikiza vimefikia kiwango cha kutovumilika. Matamko mengi yanayotolewa na viongozi wa juu wakiwamo mawaziri dhidi ya watetezi na asasi za haki za binadamu nchini yanaonyesha kuwa ni viashiria vya vitisho vya kiusalama wazi wazi kwa watetezi nchini. Pia watetezi wamekuwa wakishutumiwa kuwa ni wapinzani kwa sababu kazi zao zimekuwa zikilinganishwa na kazi za vyama vya upinzani na za kiuchochezi.

 Kuwa mtetezi ni kiungo muhimu katika kuibua na kufichua maovu ili kujenga utawala unaoheshimu haki za binadamu, lakini siku zote tumejikuta tukihatarisha maisha yetu. Katika mazingira ya aina hiyo watetezi hawawezi kujiweka katika kundi salama hata kidogo, bali kwamba usalama wao umo hatarini kwa sababu kazi nyingi wanazozifanya huwalazimisha kuikosoa serikali pale inapokuwa haitimizi wajibu wake kuhusiana na kulinda haki za msingi za binadamu na haki nyinginezo stahiki.  Mifano halisi ya migongano kati ya asasi na serikali ni kesi za kugombea ardhi Pugu, Loliondo, Bagamoyo na migogoro isiyoisha katika migodi mkoani Mara. 

2.      Wamiliki wa vyombo vya habari

Katika kudadisi ni kwa nini wanahabari wanakabiliwa na changamoto nyingi za kiusalama iligundulika kwamba wamiliki wa vyombo hawana mikakati mizuri juu ya suala zima la usalama kwa waandishi wao. Pia malipo finyu kwa wanahabari ilionekana  kuchangia kwa kiasi kikubwa kwa sababu baadhi yao hawapati malipo ya uhakika wala mikataba. Hali hiyo husababisha waandishi waishi maisha ya kubahatisha na wakati mwingine hujikuta wakishawishika kuingia katika makundi ya kisiasa  ili kuanza kuvitumikia ‘vyanzo vyao’ jambo ambalo husababisha wakiuke maadili ya kazi zao na mwisho hushambuliwa na wale wanaoguswa na habari za aina hiyo. Aidha watetezi wanawasihi wamiliki kuanza kuweka mikakati ya kiusalama kwa waandishi na kuboresha mishahara kwa waandishi ili wafanye kazi kwa uhakika zaidi.  


3.      Jeshi la Polisi

Jeshi la Polisi wawe makini na matumizi ya silaha za moto na nguvu za ziada ambazo zimekuwa zikisababisha vifo na ulemavu wa kudumu. Katika purukashani nyingi za kisiasa jeshi hilo limeshindwa kabisa kuonyesha kwamba linafanya kazi ya kuutumia umma wa Watanzania wote na badala yake limekuwa likichukua mwelekeo wa kuwatumikia wanasiasa au chama fulani. Aidha askari polisi  wanakumbushwa kwamba wao ni sehemu ya jamii na hao wanaowatesa ni ndugu zao wa karibu wadogo zao mama zao n.k. Jeshi la Polisi litambue kuwa kazi za watetezi wa haki za binadamu ni kazi halali zinazolindwa kisheria na wanajukumu la kuweka mazingira mazuri ya watetezi kufanya kazi zao bila kutekwa, kuteswa ama kungo’lewa macho,  meno, kucha n.k. Mfano halisi wa mapungufu ya jeshi hilo ni kukamatwa kwa askari hivi karibuni waliokuwa na fuvu la kichwa cha mtu mkoani Morogoro kwa lengo la kumbambika mtu kesi ya jinai. Tunaisihi Serikali na Jeshi la Polisi kuanza kutekeleza Tamko la Umoja wa Mataifa la tarehe 15 Machi 2013 linalotaka mataifa yote kutambua umuhimu na uhalali wa majukumu ya watetezi wa haki za binadamu katika kutetea haki za binadamu demokrasia, utawala wa sheria, kama nyenzo la kuhakikisha usalama wao ikiwa ni pamoja na kuheshimu uhuru wa asasi zao na kuepuka kunyanyapaa shughuli za asasi za kiraia.  



4.      Wanaharakati na Watetezi wa Haki za Binadamu 

Wanaharakati wote na watetezi wa haki za binadamu wasichukue upande wowote katika masuala ya itikadi za kisiasa kwani wao ni watu wa kati. Pia wanaharakati wasijiingize katika matumizi ya nguvu au kupambana na Jeshi la Polisi. Aidha wanaharakati wametakiwa kuwa waelimishaji wa umma na kujizuia kujiingiza katika mambo yaliyopandikizwa na watu wasioitakia mema nchi yetu kama vile udini na migogoro isiyoisha ya kugombea ardhi, maeneo ya malisho,  ukabila n.k.


5.      Vurugu za Udini

Kwa miaka mingi Tanzania haikuwahi kupata misukosuko ya udini kama inayotokea sasa. Lakini kwa miaka ya hivi karibuni uhasama wa kidini umezidi kushamiri. Watetezi kwa umoja wetu tunaamini Tanzania hatuna udini bali kinachoendelea ni ajenda za watu fulani kwa maslahi binafsi ama ya kifedha, kidini au kisiasa. Kwa sasa nchi inaweza kutumbukia katika machafuko ya kidini endapo viongozi wa dini zote, wanasiasa na serikali hawatachukua hatua za makusudi kuwakomesha wachache hao ambao wanataka kuondoa amani ya nchi. Katika mazingira haya pia mtetezi wa haki  za binadamu hawezi kubakia salama na ndio maana tunakemea kwa nguvu zote vitendo hivi viovu.


6.      Watanzania Wote Kwa Ujumla


Watanzania katika ujumla wao wameaswa kuwa makini hususani wakati huu tunapoelekea katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Wapo watu wanaochomekea ajenda zao kwa malengo wanaoyafahamu wao wenyewe na hivyo kuligawa taifa katika misingi ya udini na mambo mengine kama hayo yasiyo na tija wala manufaa kwa nchi yetu. Aidha Watanzania wameshauriwa kuirejea kazi nzuri ya kuwaunganisha ambayo iliifanya nchi hii ifahamike kama kisiwa cha amani miongoni mwa Jumuiya ya Kimataifa.


Mwisho tunaungana na watanzania wengine kulaani kitendo cha kutupa mabomu katika mikusanyiko ya watu kama ilivyotekea kule Arusha. Tunawapa pole wafiwa na majeruhi wote. Na kutaka watanzania wote bila kujadili itikadi zao kuendelea kulaani vitendo hivi vya kinyama.
TAMKO HILI LIMEANDALIWA NA WATETEZI 30 WA HAKI ZA BINADAMU TOKA MIKOA MBALIMBALI KWA NIABA YA WENZAO KATIKA AZIMIO LA KUIREJESHA NCHI HII KATIKA HALI YA AMANI NA UTULIVU

KWA PAMOJA TUTAFANIKIWA TUNAOMBA MSAADA WAKO.





Taasisi ya kuhamasisha maendeleo na mawasiliano katika jamii yenye makao yake mjini Musoma mkoani Mara ya JAMII INFORMATION NETWORK inatarajia kufanya Kongamano kubwa litakalo wahusisha  Wanafunzi zaidi ya 200 kutoka Shule 10 za Sekondari za Manispaa ya Musoma Mwezi August Mwaka huu, ikiwa ni njia ya kuhamasisha Maendeleo na kuimarishaji wa Mawasiliano ndani ya Jamii.

Katika Kongamano hilo mada mbalimbali zitatolewa na Wataalamu waliobobea katika Masuala uhamasishaji wa Vijana Kupambana dhidi ya Ukimwi,ujasiriamali,dhana ya kujiajiri,Changamoto katika Elimu kwa Vijana  pamoja na Ukatili wa Kijinsia ikiwa ni njia ya kujenga Msingi bora wa Makuzi kwa Vijana wetu.

Mbali na hivyo vijana hao pia wataelezwa jinsi ya kuwa Wazalendo katika nchi yao,kupambana na rushwa,Umaskini lakini pia wakipata elimu sahihi ya faida za uwekezaji kwa Tanzania,Sababu za Mimba za Mapema kwa watoto wa kike na jinsi ya kujenga Mahusiano na Mawasiliano yaliyo sahihi.

Pamoja na Mtandao huu kuwa na nia njema katika kuwasaidia Vijana lakini bado kumekuwepo na Changamoto mbalimbali katika kufanikisha Kongamano hilo hasa katika Suala la kifedha,hivyo basi Taasisi ya JAMII INFORMATION NETWORK kwa nia njema inakuomba wewe Mtanzania,Mpenda Maendeleo,unaekaa ndani au nje ya nchi,Mashirika kusaidia Taasisi hii katika kufanikisha Kongamano hilo ili vijana wetu wakue katika Makuzi mema na kujenga Tanzania ya kesho  iliyostaarabika.

 Blog Master

ASKARI ALIYEUA TARIME CHINI YA ULINZI

Mwanafunzi mmoja wa darasa la kwanza katika shule ya msingi rebu wilayani tarime mkoani mara deus jacob,ameuawa kinyama baada ya kupigwa risasi kichwani na askari polisi wa  wilayani tarime  wakati  wakiwa katika harakati za kumkamata  mtuhumiwa wa kosa la kushambulia na kujeruhi.
 
kamanda wa polisi kanda maalum ya tarime rorya,kamishina msaidizi  justus kamugisha,amesema mwanafunzi huyo mkazi wa songambele wilayani tarime amepigwa risasi hiyo ambayo imesababisha kupoteza maisha na askari polisi mwenye namba d 4662 koplo methew  wakati akipita barabarani.
 
kamanda kamugisha amesema kuwa risasi hiyo ambayo imemuawa mwanafunzi huyo ni miongoni mwa risasi tano ambazo zilifyatuka wakati wa porukushani  ikihusisha mtuhumiwa  huyo marwa chacha na  askari polisi katika jaribio la kupora bunduki.
 
kwa mujibu wa kamanda kamugisha  askari polisi huyo anashikiriwa kwa mahojiano wakati wakimtafuta mtuhumiwa marw chacha  ambaye alikimbia baada ya tukio hilo kutokea  ambapo polisi walifanikiwsa kukamata misokoto ya bangi 45 na kilo 3 na roba za bangi kavu ambayo inadaiwa ni mali ya mtuhumiwa huyo.
 
kwa upande wake mzazi wa mwanafunzi huyo mzee jacob mwita sasi,amelaani kitendo cha polisi huyo kumua mtoto wake kwa risasi bila kosa hivyo kutaka vyombo vya sheria kuchukua harua ili kuhakikisha haki inatendeka.

MUHIMU KWA WADAU WA BLOG HII! NDANI NA NJE YA NCHI

Mpendwa Msomaji wa blog hii ya JAMII INFORMATION NETWORK tunashukuru sana kwa kuitembelea Blog hii ambayo ni blog  inayomilikiwa na Taasisi ya JAMII INFORMATION NETWORK  (JIN) inayojihusisha na Uhamasishaji wa Maendeleo na Mawasiliano katika Jamii.

Blog hii itakuwa ikikueleza matukio mbalimbali ya Kijamii ambayo yatakuwa yanaigusa Jamii moja kwa moja au kwa njia nyingene  na pia kuibua changamoto zilizopo katika Jamaii yetu,Hivyo basi tunaomba utuunge Mkono katika kuitazama blog hii.

Blog Editor

POLISI WAUA TARIME MTOTO WA MIAKA 9 KWA RISASI

Haya ndiyo yaliyofanyika Tarime leo mtoto wa miaka 9 kuuuwa na jeshi la polisi kwa uzembe eti wanawakamata majambazi ambao si wale wanaoiba na kuuwa watu mpaka mwa Tanzania na Kenya kashuhudie mwenyewe uone then comment! hATA HIVYO UNAOWAONA NI WANANCHI WALIOCHOKA WAKIANADAMANA HUKU WAMEBEBA KWENYE MACHELA MWILI WA MAREHE dEO yKOB MWNAFUNZI WA DARASA LA TATU KATIKA SHULE YA MSINGI MTURU MJINI HAPA! Nimelishuhudia hili.

MLEMAVU WA NGOZI (ALBINO) ASIMAMISHWA SHULE KWA KUTUHUMIWA KUWA MSHIRIKINA MLOWO MBOZI

Hapa Amina akimsimulia mkasa mzima mwandishi wa Mbeya yetu Joseph Mwaisango mara baada ya kupata maelezo yote ya Amina mwandishi wetu alimpigia simu katibu wa chama cha maalbino mkoa wa Mbeya afike ofisi ya Mbeya yetu ili wasaidiane kutatua tatizo hilo
katibu wa Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya, Wiliamu Simwale alifika ofisi ya Mbeya yetu na kuanza kumsikiliza Amina
katibu wa Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya, Wiliamu Simwale akiwa makini kumsikiliza Amina katika ofisi ya Mbeya yetu

KATIKA Hali isiyokuwa ya Kawaida Uongozi wa Shule ya Sekondari Hollwood iliyoko Mlowo Wilayani Mbozi Mkoa wa Mbeya imemsimamisha shule Mwanafunzi wa kidato cha tatu kwa takribani Miezi Miwili kwa madai kuwa anajihusisha na imani za Kishirikina.

Mwanafunzi huyo aliyejulikana kwa jina la Amina Mwankinga(20) ambaye ni mlemavu wa ngozi(Albino) alisimamishwa shule na uongozi wa Shule hiyo tangu Machi 9, Mwaka huu baada ya uongozi wa Shule hiyo kupata taarifa kutoka kwa Wanafunzi wakimtuhumu Mwenzao huyo kuwa ni Mshirikina.


Uongozi wa Shule hiyo baada ya kupata taarifa hizo ulimwamuru mhanga wa tukio hilo kuondoka Shuleni hapo pasipo kufuatilia na kujua ukweli wa jambo hilo na kupata udhibiti hivyo kumwacha Mwanafunzi huyo akizurura mitaani asijue hatma ya maisha yake.


Mhanga wa tukio hilo Amina Mwankinga alisema tangu tarehe tisa alipofukuzwa bwenini na wanafunzi wenzie wakitaka aondoke shuleni hapo majira ya usiku hali iliyomlazimu kuomba hifadhi kwa mlinzi aliyemkubalia na kukesha naye hadi asubuhi hali iliyopelekea kupigwa na baridi kali kutokana na kukosa nguo za kujisitiri kama Shuka nk.


Anasema kutokana na hali hiyo Walimu pamoja na uongozi wa Shule hiyo haukuchukua hatua yoyote jambo lililomlazimu kuondoka Shuleni hapo baada ya kukosa msaada ambapo alirejea Jijini Mbeya anakoishi na Binamu yake.


Binti huyo anayesomeshwa na Shirika la Under the SameSun iliyoko Jijini Dar Es Salaam aliwaambia waandishi wa habari kuhusu mkasa uliompata huku akiomba msaada kwa wasamaria wema kumtafutia Shule ili aendelee na masomo kwa ajili ya kujiandaa na mtihani wa kidato cha nne Mwakani.


Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya HollyWood Ambukeghe Mtafya, alipopigiwa simu kuhusu tuhumahizo alikiri kulijua suala hilo na kwamba walimrudisha mwanafunzi huyo nyumbani ili kumnusuru na kipigo kutoka kwa wanafunzi wenzie na kuongeza kuwa aliambiwa atafute shule nyingine ili ahamie.


Naye katibu wa Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya, Wiliamu Simwale alisema alikuwa halijui suala hilo na kwamba kama lingekuwa suala liko nyeti angejulishwa yeye juu ya hatua zilizofikiwa ambapo Uongozi wa Shule umeendelea kupokea fedha za malipo ya Mwanafunzi pasipo kutoa taarifa kwenye shirika linalolipa.


Mlezi wa Wanafunzi hao kutoka Shirika la Under the Samesun Omary Mfaume amesema kwamba hana taarifa zozote kuhusiana na tukio hilo na kuongeza kuwa anawasiliana na uongozi wa Shule moja kwa moja ili umweleze juu ya kilichotokea ili taratibu za kumtafutia Shule nyingine zifanyika haraka ili Mwanafunzi aendelee na masomo kama kawaida.


Source  Mbeya yetu
Like us on Facebook
Follow us on Twitter
Recommend us on Google Plus
Subscribe me on RSS